Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2021

Swalah ya Kuomba Mvua

 SWALAH YA KUOM BA MVUA Taarif (Maana ) yake   “Al-Istisqaa” ni kumwomba Allaah Aiteremshe mvua wakati wa ukame. Maulamaa wote wamekubaliana kwamba hilo ni Sunnah aliyoiweka Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihiy wa sallam), lakini wamekhitalifiana kuhusiana na Swalaah yenyewe kama tutakavyobainisha.   Hukmu ya Swalaah ya Kuomba Mpya    Ukame ukiingia, ardhi ikakauka na mvua ikapotea, imesuniwa imamu atoke pamoja na watu hadi sehemu maalumu ya kuswalia kama tutakavyoeleza, kisha aswali nao rakaa mbili. Hili ndilo lililothibiti toka kwa Nabiy wa Allaah  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).   Imepokelewa toka kwa ‘Abbaad bin Tamiym toka kwa ami yake akisema: “Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka kwenda sehemu ya kuswalia kwa ajili ya kuomba mvua. Alielekea Qiblah na kuswali rakaa mbili na akageuza nguo yake kwa kupindua kulia kuja kushoto.”   [ Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy]. ...

Maswali Mchanganyiko kuhusu Swalah ya Kusuwf (Swalah ya Kupatwa kwa Jua/Mwezi

  Je, Husomwa Hwa Sauti Au Kimya Kimya?   Ahmad, Is-Haaq na Maswahibu wawili wa Abu Haniyfah wanasema kwamba ni Sunnah kusoma kwa sauti kinyume na Jamhuri. [Rejea zilizotangulia kuhusiana na namna ya kuswali] Dalili zao ni:   1-  Hadiyth ya ‘Aaishah asemaye: “Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma kwa sauti katika Swalaah ya Khusuwf. Anapomaliza kusoma, hupiga takbiyr akarukuu, na anaponyanyuka toka kwenye rukuu husema: “Sami’a Allaahu liman hamidahu, Rabbanaa walakal Hamdu”. Kisha hufanya tena kisomo katika Swalaah ya Kusuwf rukuu nne katika rakaa mbili na sijdah nne” .  [ Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1065)].   2- Ni Naafilah iliyoruhusiwa kuswaliwa kwa jamaa. Hivyo basi, sehemu ya Sunnah yake ni kusomwa kwa sauti kama ilivyo kwa Swalaah za ‘Iyd, Tarawehe na Kuomba Mvua.   Jamhuri wamesema: “Husomwa kwa sauti katika Swalaah ya Kupatwa Mwezi tu, ama Kupatwa Jua haisomwi kwa sauti”. Hoja yao ni:  ...

Picha ya Namna ya Kuswali swalah ya Kupatwa kwa Jua/Mwezi

Picha ya Swalaah ya Kusuwf Kwa Muhtasari   1- Apige takbiyr, asome du’aa ya ufunguzi, asome isti’aadhah, asome Al-Faatihahh, na kisha asome kiasi cha Suwrat Al-Baqarah.   2- Arukuu rukuu ndefu.   3- Anyanyuke toka kwenye rukuu na aseme: “Sami’a Allaahu liman hamidahu, Rabbanaa walakal Hamdu”.   4- Asisujudu, bali asome Al-Faatihah na Suwrah fupi kidogo kuliko ile ya kwanza.   5- Arukuu tena rukuu ndefu na apunguze kidogo urefu kulinganisha na ile ya kwanza.   6- Anyanyuke toka kwenye rukuu na aseme: “Sami’a Allaahu liman hamidahu, Rabbanaa walakal Hamdu”.   7- Asujudu, kisha akae, halafu asujudu tena.   8- Anyanyuke kwenda rakaa ya pili, kisha afanye kama alivyofanya katika rakaa ya kwanza. Inaendelea..... Na Allaah anajua zaidi 

Aina nyingine za Kuswali Swalaat Kusuwf

AINA NYINGINE ZA NAMNA YA KUSWALI SWALAH YA KUPATWA KWA JUA/MWEZI  Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh  Imehadithiwa kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliiswali kwa miundo mingineyo. Kati yake ni:   3- Kila rakaa rukuu tatu [ Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (901), Abu Daawuud (1177) na An-Nasaaiy (3/129) toka kwa ‘Aaishah] .   4- Kila rakaa rukuu nne [ Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (908) na Abu Daawuud (1183)]. Ibn Al-Qayyim anasema: “Maimamu wakubwa hawalioni hilo kuwa ni sahihi, bali wanaliona ni kosa kama Al-Imaam Ahmad, Al-Bukhaariy na Ash-Shaafi’iy”.  [ Zaadul Ma’ad (1/453) chapa ya Ar-Risaalah]   Ninasema: “ Utendaji sahihi zaidi wa Swalaah hii ni kufanya rukuu mbili katika kila rakaa kama walivyosema Jamhuri kutokana na uwazi wa Hadiyth Swahiyh husika. Ama dalili za Abu Haniyfah na waliokubaliana naye, dalili hizi zimetaja rakaa mbili bila uainisho wakati Hadiyth za kundi la kwanza zimeainisha”.   Ama Hadiyth ya ...

Namna ya Kuswali Swalat Kusuwf (Swalah ya Kupatwa kwa Jua/Mwezi

  NAMNA YA KUSWALI SWALAH YA KUPATWA KWA JUA/MWEZI  Swalaah ya Kusuwf ni rakaa mbili tu, hakuna mabishano kati ya Maulamaa kuhusu hili. Walilobishania ni utendaji wake kwa kauli tofauti. Zilizo mashuhuri zaidi ni mbili:   Ya kwanza:   Ni rakaa mbili. Kila rakaa ina visimamo viwili, visomo viwili, rukuu mbili na sijdah mbili. Wanaosema haya ni Maalik, Ash-Shaafi’iy na Ahmad. [ Ad-Dusuwqiy (1/405), Al-Ummu (1/215), Kash-Shaaful Qinaa (2/62) na Al-Mughniy (2/422)]   Dalili zao ni:   1-  Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliyesema: “Jua lilipatwa wakati wa enzi ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nabiy akaswali pamoja na watu. Akasimama kisimamo kirefu cha kiasi cha kusoma Suwrat Al-Baqarah. Kisha alirukuu rukuu ndefu, halafu akasimama kisimamo kirefu chini kidogo ya kisimamo cha kwanza. Kisha alirukuu rukuu ndefu chini kidogo ya rukuu ya kwanza”.  [ Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1046) na Muslim (901)].   2- ...

Sunnah katika Swalah ya Kusuwf (Kupatwa kwa Jua /Mwezi

    YALIYOSUNIWA KWA MWENYE KUSHUHUDIA KUSUWF (KUPATWA KWA JUA /MWEZI   1- Akithirishe dhikri, kuomba maghfirah, kupiga takbiyr, kutoa swadaqah na amali nyingine njema.   ‘ Aaishah anasema kwamba Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: ((Mtakapoona hilo, basi mwombeni Allaah, pigeni takbiyr, swalini na toeni swadaqah)) .  [ Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1044) na Muslim ( 901)].   Na  Asmaa anasema: “Hakika Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniamuru nimwache huru mtumwa jua lilipopatwa”.  [ Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1056) na Muslim (903)].   2- Aende kuswali kwa Jamaa Msikitini   Hadiyth ya ‘Aaishah inaeleza: “Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipanda asubuhi kipando (mnyama), jua likapatwa, akarejea dhuhaa. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapita baina ya vyumba, kisha akasimama na kuswali”. ...

Swalaat Kusuwf (Swalah ya Kupatwa kwa Jua

  SWALAAT KUSUWF/KHUSUWF (SWALAH YA KUPATWA KWA JUA na MWEZI Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh  Naam Leo tunaendelea na Darsa zetu katika Group zetu za Whatssap na katika Blog yetu hii ya BUSTANI YA ELIMU pamoja na page zetu ndani ya Facebook.. Maana ya Kusuwf ✅Naam neno Kusuwf ni kupotea mwanga wa jua au mwezi au sehemu ya mwanga na kubadilika kuwa weusi, na “Khusuwf” ni kisawe(Kinyume) chake.  ➡️Ama Wataalamu wengine wanasema kwamba “Kusuwf” ni kupatwa jua na “Khusuwf” ni kupatwa mwezi, na tafsiri hii ndiyo mashuhuri zaidi katika lugha.  ↪️Rejea Kitaab Lisaan Al-‘Arab, Kash-Shaaf Al-Qinaa (2/60) na Asnaa Al-Matwaalib (1/385). ✅Swalaah ya  “Kusuwf” ni Swalaah inayoswaliwa kwa mtindo maalumu wakati jua au mwezi ukipatwa wote au sehemu.  ↪️Rejea Kitaab Mawaahibul Jaliyl (2/199), Nihaayatul Muhtaaj (2/394) na Kash-Shaaful Qinaa (2/60). Wakati/Muda wa Kuswali Swalah ya Kusuwf   ✅Ni kuanzia pale jua linapoanza kupatwa mpaka linapoachiliwa kutoka...