Adabu za Ndoa
Adabu za Ndoa katika Sunnah MKE NA MUME KUOGA PAMOJA Inaruhusiwa kwa mume na mke kukoga pamoja katika sehemu moja hata kama mume ataona sehemu za siri za mke na mke ataona sehemu za siri za mumewe. Hii imethibitika katika Hadiyth Swahiyh mbali mbali, miongoni mwa hizo ni: Kwanza : عَنْ عَائِشَة ، قَالَتْ: كُنْتُ أَغْتَسِلُ أَنَا وَرَسُولُ اللّهِ مِنْ إِنَاءٍ. ـ بَيْنِي وَبَيْنَهُ ـ، وَاحِدٍ (تختلف أيدينا فيه). فَيُبَادِرُنِي حَتَّى أَقُولُ: دَعْ لِي، دَعْ لِي. قَالَتْ: وَهُمَا جُنُبَانِ Imetoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها ambaye alisema: "Nilikuwa nakoga na Mtume kutoka chombo kimoja cha maji kilichowekwa baina yetu (kiasi kwamba mikono yetu ilikuwa ikipishana katika maji). Alikuwa akishindana na mimi hadi nikasema: Nibakishie (maji), nibakishie (maji)". Akaongeza: "Tulikuwa katika hali ya janaba" (yaani hali ya kutoka katika tendo la ndoa ) Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim Pili: عن معاوية بن...