Machapisho

Tafsiyr Ya Imaam As-Sa'dy Kuhusu Kufaridhishwa Swawm

 Naam  Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:       يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ   ﴿١٨٣﴾ Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa.  [Al-Baqarah: 183]   Allaah Anajulisha katika Aliyoyafadhilisha kwa waja Wake kwamba Amewajibisha Swawm kama Alivyowajibisha ummah zilizopita kwa sababu ni  shariy’ah  (hukmu) na amri zinazomnufaisha bin Aadam katika kila zama.   Nayo ni changamoto ya kumhuisha mtu nafsi yake kwani inapasa kushindana na wengine katika mambo ya khayr ili mkamilishe 'amali zenu na mkimbilie (kuchuma) sifa njema na hakika hayo si katika mambo mazito mliyohusishwa nayo.   Kisha Allaah Anataja hikma Yake kuhusu  Shariy’ah  ya Swawm, Anasema: لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ mpate kuwa na taqwa   kwamba Swawm ni sababu kuu ya taqwa (kumcha Allaah) kwa kuwa ...

Makosa yafanywayo na wenye Swawm Katika Mwezi wa Ramadhwaan

 Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh  Yafuatayo ni makosa ambayo yameonekana yakitendeka katika mwezi wa Ramadhwaan ima wanapokuwa Waislamu katika Swawm au baada ya kufuturu na katika Swalah za Qiyaamul-Layl. Hivyo inapasa tuyazingatie na kujiepusha nayo ili tubakie katika usalama wa Swawm zetu, Swalah zetu na mengine yote yanayohusu mwezi huu mtukufu:    1. Kutia Niyyah Kwa Kutamka:   Baadhi wanaamini kuwa niyyah usipoitamka basi haijawa niyyah. Na pia huwafunza watoto kutamka maneno ya kutia niyyah, au kuwaamrisha wasikose kwenda kunuizwa Msikitini na mashekhe. Itambulike kuwa niyyah mahali pake ni moyoni na kutamka ni uzushi.     2. Kufunga bila kuswali:   Baadhi ya watu wanafunga bila ya kuswali au kutimiza Swalah ipasavyo. Watu kama hawa Swawm zao hazifai kwani Swalah ni nguzo ya Dini ya Kiislamu.   3. Kudhani kwamba Swalah ya Taraawiyh inaanzwa siku ya kwanza ya Ramadhwaan: Hali inaanza usiku ule unaoandama mwezi. Sunnah n...

Ramadhwaan ni Mwezi wa Du’aa na Du’aa hutakabaliwa

  Du’aa ni ‘ibaadah kama ilivyothibiti katika Hadiyth:     عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي قَوْلِهِ  ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ))  قَالَ: ((الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ)) وَقَرَأَ  ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ))  إِلَى قَوْلِهِ:  ((دَاخِرِينَ)) Amesimulia Nu’maan bin Bashiyr  (رضي الله عنه)   kwamba Nabiy ( صلى الله عليه وآله وسلم ) kuhusu kauli yake [Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa]:  وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ((Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni))   Amesema: ((Du’aa ndio ‘ibaadah)) kisha akasoma:    وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ  ۚ  إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ  دَاخِرِينَ﴿٦٠﴾ Na Rabb wenu Amesema: Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari katika kuniabudu wataingia Jahanam wadhalilike. ...