Fisadi Gani Mbili za Mayahudi zilizotajwa katika Suwrat Bani Israaiyl?
SWALI: Assalam alaykum Natumai mnaendelea vizuri na afya njema na shughuli zenu za Dawa. Ningependa kuuliza: Katika kitabu kitukufu Qur'an, Allaah ameelezea katika Suwrah Al-Israa au Bani Israel katika aayah ya 4 - 5. Napenda kujua hizo fisadi mbili zilizoandikwa kuwa Wana wa Israel watazifanya, haswa hiyo ya kwanza ilitokea wakati gani na wakati wa Nabiy gani. Na ni watu gani katika waja wake Allaah ambao aliwapeleka kuwatia adabu. Kisha napenda kujua hiyo fisadi ya pili ni ipi au lini itatokea. Na kama kuna mengine ya ziada tuchambulini kwa hawa watu ambao Allaah amewalaani kwa jeuri yao. Shukran JAWABU: Hakika hili ni swali nyeti ambalo inatakiwa kila Muislamu awe na ufahamu nalo. Swala la Mayahudi ambao Qur-aan, Hadiyth za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hata historia imetubainishia uovu wao usio kifani. Lakini hapa si mahali pake kuelezea hayo kwani swali mbele yetu ni jengine japokuwa linahusiana. Hakika ufisadi wa...