Mwenye Hedhi kuingia Msikitini na Hukmu ya Kupata Hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja?
*Swali*
A
ssalam Alleykum je inajuzu mwanamke mwenye hedhi kuingia msikitini kwa ajili ya kusoma ?? je nikipimo gani kishilia kutenganisha dam ya hedhi na homa au ni masiku mangapi kwa mwanamke yakipita utasema dam hii ni hedhi na sasa ni homa akaswali na kusoma quani ?? au mwanamke kupata hedhi mala mbili kwa mwezi mmoja nini jukum yake ??
*Jawabu*
Wa Aleykum Salaam WarahmatulLaah Wabarakatuh...
✅Naam nakumbuka katika Kitaab Fiqh'i Sunnah-Mlango wa Twahara nilielezea kwa Mapana sana kuhusiana na Masuala ya Damu ya Hedhi na Hukmu zake..
➡️Kwa kifupi sana Ni damu nyeusi, nzito na yenye harufu mbaya. Inamtoka mwanamke toka sehemu maalumu katika nyakati maalumu.
➡️Damu ya hedhi haina mpaka wa uchache wala wingi, bali hilo linategemea maumbile ya mwanamke, kwa vile hakuna dalili yoyote sahihi toka kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inayobainisha uchache wake au wingi wake.
Kwahiyo Damu ya Hedhi inaweza ikakatika kwa siku 1 au 2 au 4 na wengine hadi siku 7 kutegemeana na Mwanamke..
➡️Mwanamke hawezi kupata Hedhi mara 2 ndani ya mwezi mmoja, ikitokea hivyo basi Mwanamke huyu atakuwa na Matatizo ya Kiafya ama Damu inayokuja mara pili huwa ni Damu ya Ugonjwa Kisheria huwa inaitwa Damu ya Istihaadhwah (yaani Damu yenye Kuendelea baada ya Hedhi kukata)
NB: Mwenye Damu ya Istihaadhwah Kisheria anaruhusiwa kufanya Ibada zote , hivyo atafanya Wudhuu kila Wakati wa Ibadah.
✅Na Wanachuoni wanasema ya kwamba kuna tofauti tatu kati ya damu ya damu ya ugonjwa na hedhi⤵️
1- Damu ya hedhi ni nyeusi tofauti na istihaadhah ambayo ni nyekundu.
2- Damu ya hedhi ni nene tofauti na istihaadhah ambayo ni nyembamba.
3- Damu ya hedhi inanuka tofauti na istihaadhah.
✅Kuhusu Mwenye Hedhi kuingia msikitini, Maulamaa wamekhitalifiana N wengine wamesema kuwa Inafaa kwa mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi kusoma Qur-aan kutokana na maoni sahihi zaidi ya wanazuoni kwa sababu ya kutokuwepo chenye kujulisha juu ya makatazo ya kufanya hivo.
➡️Lakini afanye hivo bila kugusa msahafu. Inafaa kwao wawili kuigusa nyuma ya kizuizi kama mfano wa nguo safi na mfano wake. Vivyo hivyo inahusu karatasi aliyoandika Qur-aan ndani yake wakati wa haja ya kufanya hivo.
➡️Kuhusu mwenye janaba haifai kwake kusoma Qur-aan mpaka akoge. Kwa sababu kumepokelewa Hadiyth Swahiyh inayofahamisha juu ya kukataza.
➡️Haijuzu kumlinganisha mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi juu ya mwenye janaba.
➡️Kwa sababu muda wao unarefuka tofauti na mwenye janaba ambaye kuna wepesi kwake kuoga katika wakati wowote kuanzia pale anapomaliza kutoka katika yale mambo yanayowajibisha janaba.
➡️Kumepokelewa Hadiythi kwamba Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema⤵️
“Mimi sikuhalalisha Msikiti kwa mwenye hedhi wala janaba.”
↪️Imepokelewa na Imaam Muslim
Kwa faida zaidi Rejea Viitaab vifuatavyo:-
(i)Kitaab Ad-Dimaa' at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa'.
(ii)Kitaab Nuur ´alaad-Darb (377).
(iii)Kitaab Majmuu´-ul-Fataawaa (10/208).
(iv)Kitaab Al-Liqaa´ ash-Shahriy (61).
(v)Kitaab Jaami'u Ahkaamin Nisaa (1/200).
(vi)Kitaab Al-Muhalla (2/191).
(vii)Kitaab Al-Mughniy (1/308).
✅Maelezo hayo yote nimeyatoa katika Vitabu hivyo nilivyovitaja hapo juu, ukipata wasaa vitafute na Usome kwasababu humo kuna Maelezo ya kutosha, WabiLaah Tawfiq.
Na Allaah anajua zaidi
_Unaruhusiwa Kusambaza, Kuwa Muadilifu, Tafadhali Usibadili Chochote_
Imeandaliwa na *Imaam Masjid Tawbah*
Maoni
Chapisha Maoni