Adabu za Ndoa

 Adabu za Ndoa katika Sunnah


MKE NA MUME KUOGA PAMOJA


Inaruhusiwa kwa mume na mke kukoga pamoja katika sehemu moja hata kama mume ataona sehemu za siri za mke na mke ataona sehemu za siri za mumewe. Hii imethibitika katika Hadiyth Swahiyh mbali mbali, miongoni mwa hizo ni:

 

Kwanza:

 

عَنْ عَائِشَة ، قَالَتْ: كُنْتُ أَغْتَسِلُ أَنَا وَرَسُولُ اللّهِ مِنْ إِنَاءٍ. ـ بَيْنِي وَبَيْنَهُ ـ، وَاحِدٍ (تختلف أيدينا فيه). فَيُبَادِرُنِي حَتَّى أَقُولُ: دَعْ لِي، دَعْ لِي. قَالَتْ: وَهُمَا جُنُبَانِ

 

Imetoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها ambaye alisema: "Nilikuwa nakoga na Mtume kutoka chombo kimoja cha maji kilichowekwa baina yetu (kiasi kwamba mikono yetu ilikuwa ikipishana katika maji). Alikuwa akishindana na mimi hadi nikasema: Nibakishie (maji), nibakishie (maji)". Akaongeza: "Tulikuwa katika hali ya janaba" (yaani hali ya kutoka katika tendo la ndoa) Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim 


Pili:

 

عن معاوية بن حدِّهِ ، قَالَ: قُلْتُ يَا نَبِيَّ الله عَوْرَاتُنَا مَا نَأْتِي مِنْهَا وَمَا نَذَرُ؟ قَالَ:  ((احْفَظْ عَوْرَتَكَ إِلاَّ مِنْ زَوْجَتِكَ أَوْ مَا مَلَكَتْ يَمِينُكَ)). قُلْتُ: يَا رَسُولَ الله إذَا كَانَ الْقَوْمُ بَعْضُهُمْ في بَعْضٍ؟ قَالَ ((إِنِ اسْتَطَعْتَ أَنْ لاَ يَرَاهَا أَحَدٌ فَلاَ تُرِيَنَّهَا)) قَالَ قُلْتُ يَا نَبِيَّ الله إِذَا كَانَ أَحَدُنَا خَالِياً؟ قَالَ ((فَالله أَحَقُّ أَنْ يُسْتَحْيَى مِنْهُ مِنَ النَّاسِ))

 

Kutoka kwa Mu'aawiyah Ibn Haydah ambaye alisema: "Nilimwambia Ee Mjumbe Wa Allaah, sehemu gani ya tupu zetu zinaruhusiwa na zipi tujihadhari nazo?" Mtume akasema: "Chunga utupu wako isipokuwa kwa mkeo au wale iliyomiliki mikono yako ya kuume" Nikasema: "Ee Mjumbe wa Allaah, je, Vipi inapokuwa jamaa wanaishi pamoja?" Mtume akasema: "Ikiwa utahakikisha kuwa hakuna mtu atakayeona tupu zenu, basi fanya hivyo". Akasema: "Ee Mjumbe wa Allaah, je, vipi inapokuwa mmoja yuko pekee (amekaa uchi)?" Mtume akasema: "Allaah Anastahiki staha zaidi ya watu wengine”Ahmad, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na wengineo: Swahiyh


Na Allaah anajua zaidi 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Eda: Maana ya Eda, Hikma ya Eda , Hukmu zake, Mambo yanayopasa na uyasiyopasa kwa mwenye Eda

Namna ya Kuswali Swalat Kusuwf (Swalah ya Kupatwa kwa Jua/Mwezi

Ramadhwaan ni Mwezi wa Du’aa na Du’aa hutakabaliwa