Swalaat Kusuwf (Swalah ya Kupatwa kwa Jua
SWALAAT KUSUWF/KHUSUWF (SWALAH YA KUPATWA KWA JUA na MWEZI
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Naam Leo tunaendelea na Darsa zetu katika Group zetu za Whatssap na katika Blog yetu hii ya BUSTANI YA ELIMU pamoja na page zetu ndani ya Facebook..
Maana ya Kusuwf
✅Naam neno Kusuwf ni kupotea mwanga wa jua au mwezi au sehemu ya mwanga na kubadilika kuwa weusi, na “Khusuwf” ni kisawe(Kinyume) chake.
➡️Ama Wataalamu wengine wanasema kwamba “Kusuwf” ni kupatwa jua na “Khusuwf” ni kupatwa mwezi, na tafsiri hii ndiyo mashuhuri zaidi katika lugha.
↪️Rejea Kitaab Lisaan Al-‘Arab, Kash-Shaaf Al-Qinaa (2/60) na Asnaa Al-Matwaalib (1/385).
✅Swalaah ya “Kusuwf” ni Swalaah inayoswaliwa kwa mtindo maalumu wakati jua au mwezi ukipatwa wote au sehemu.
↪️Rejea Kitaab Mawaahibul Jaliyl (2/199), Nihaayatul Muhtaaj (2/394) na Kash-Shaaful Qinaa (2/60).
Wakati/Muda wa Kuswali Swalah ya Kusuwf
✅Ni kuanzia pale jua linapoanza kupatwa mpaka linapoachiliwa kutokana na kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mnapoona vimepatwa, basi mwombeni Allaah na swalini mpaka mwanga urudi)).
↪️Hadiythi Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1060) na Muslim (904).
➡️Kuachiliwa kumefanywa kuwa ndiyo lengo la Swalaah kwa ajili ya kumtaradhi Allaah Airejeshe neema ya mwanga. Na linapoachiliwa, basi lengo la Swalaah linakuwa lishapatikana. [Vitabu rejea vilivyotangulia kuvitaja hapo juu]
Kupita/Kumalizika kwa Swalah ya Kusuwf
✅Swalaah ya Kupatwa Jua inapita kwa moja ya mawili ambayo ni haya yafuatayo⤵️
1️⃣Kurejea mwanga kamili. Ikiwa mwanga utarejea kidogo, basi inajuzu kuswali kwa sehemu iliyobakia ya giza kana kwamba hiyo ndiyo bado inayopatwa.
2️⃣Ni kuchwa jua likiwa bado limepatwa.
➡️Na Swalaah ya Kupatwa Mwezi hupita kwa moja ya mawili:
1- Kurejea nuru kamili.
2- Kuchomoza jua au kutoweka mwezi ukiwa bado umepatwa. Na ikiwa mawingu yatazuia na mtu akashakia kama umeachiwa au la, basi ataswali kwa kuwa asili ni kubakia kusuwf.
↪️Rejea Kitaab Al-Mughniy (2/427), Rawdhwat At-Twaalibiyna (2/87) na Al-Mawaahib (2/203).
Faida
✅Swalaah ya Kupatwa Jua huswaliwa wakati wowote hata katika nyakati zilizopigwa marufuku kuswali. Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy.
HUKMU YA SWALAH YA KUPATWA KWA JUA /MWEZI
✅Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba Swalaah ya Kupatwa Jua ni Sunnah iliyokokotezwa(iliyotiliwa mkazo).
➡️Lakini Abu ‘Awwaanah ameeleza kwamba ni WAJIBU kwa mujibu wa riwaya iliyopokelewa toka kwa Abu Haniyfah wakati ambapo Maalik ameichukulia kama ni Swalaah ya Ijumaa. Kauli hii ya kusema ni wajibu iliyopewa uzito na Ash-Shawkaaniy, Swiddiyq Khaan na kisha Al-Albaaniy, ina mwelekeo wa nguvu kutokana na kuthibiti maagizo ya kuiswali.
↪️Rejea Kitaab Fat-hul Baariy (2/612), As Saylul Jarraar (1/323), Ar-Rawdhwat An Nadiyyah (uk 156) na Tamaam Al-Minnah (uk.261)]
✅Ama hukmu ya Swalaah ya Kupatwa Mwezi, Maulamaa wamekhitalifiana juu ya kauli mbili ambazo ni⤵️
1️⃣Kauli ya kwanza.
✅Ni Sunnah iliyokokotezwa na huswaliwa jamaa kama Swalaah ya Kupatwa Jua. Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Daawuud, Ibn Hazm, ‘Atwaa, Al-Hasan, An-Nakh’iy na Is-Haaq. Kauli hii imehadithiwa toka kwa Ibn ‘Abbaas.
↪️Rejea Kitaab Al-Ummu (1/214), Al-Mughniy (2/420), Al-Inswaaf (2/442), Bidaayatul Mujtahid (1/160) na Al-Muhalla (5/95).
➡️Na hoja yao ni haya yafuatayo⤵️
(1)Hadiythi ya Al-Mughiyrah ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( Hakika jua na mwezi ni alama mbili kati ya Alama za Allaah. Havipatwi kwa kufa mtu wala kwa kuzaliwa, na mnapoona vimepatwa, basi mwombeni Allaah na mswali mpaka mwanga urudi)).
↪️Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1060) na Muslim (904).
➡️Kuna Hadiythi kama hii ya ‘Aaishah, Ibn ‘Umar, Ibn ‘Abaas na Abu Bakrah.
(2)Yaliyosimuliwa ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Swalaah ya Kupatwa Mwezi.
↪️Angalia Kitaab (Fat-h) (3/638)]
(3)Yaliyosimuliwa toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba aliswali na wakazi wa Basrah Swalaah ya Kupatwa Mwezi rakaa mbili kisha akawaambia: “Nimeswali hivi kwa kuwa nimemwona Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali”.
↪️Isnadi yake ni Dhwa’iyf: “Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/342). Pia Ash-Shaafi’iy kaifanyia “ikhraaj” mfano wake katika musnadi wake (484), na Al-Bayhaqiy kanukuu toka kwake (3/342) lakini Sanad yake haifai.
2️⃣Kauli ya pili.
➡️Haiswaliwi kwa jamaa, nayo ni Sunnah kama Sunnah zinginezo bila kuzidisha katika rukuu. Ni kauli ya Abu Haniyfah na Maalik.
↪️Rejea Kitaab cha Ibn ‘Aabidiyn (2/183), Al-Badaai-’i (1/282), Mawaahibul Jaliyl (2/201), Bidaayatul Mujtahid (1/312), na Ad-Dusuwqiy (1/402).
➡️Wamesema: “Ni kutokana na uzito wakati wa usiku kinyume na mchana, na kutotaarifiwa toka kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba aliiswali kwa Jamaa pamoja na kwamba kupatwa mwezi kulikuwa zaidi kuliko kupatwa jua!!
✅Ninasema: “Kauli ya kwanza ina nguvu zaidi kwa kuwa Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameagiza kuziswali Swalaah hizo mbili bila ya kufarakanisha”.
Inaendelea.......
Unaruhusiwa Kusambaza, Kuwa Muadilifu, Tafadhali Usibadili Chochote
Imeandaliwa na Imaam Masjid Tawbah
Maoni
Chapisha Maoni