Aina nyingine za Kuswali Swalaat Kusuwf

AINA NYINGINE ZA NAMNA YA KUSWALI SWALAH YA KUPATWA KWA JUA/MWEZI 


Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh 


Imehadithiwa kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliiswali kwa miundo mingineyo. Kati yake ni:

 

3- Kila rakaa rukuu tatu [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (901), Abu Daawuud (1177) na An-Nasaaiy (3/129) toka kwa ‘Aaishah].

 

4- Kila rakaa rukuu nne[Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (908) na Abu Daawuud (1183)].

Ibn Al-Qayyim anasema: “Maimamu wakubwa hawalioni hilo kuwa ni sahihi, bali wanaliona ni kosa kama Al-Imaam Ahmad, Al-Bukhaariy na Ash-Shaafi’iy”.  [Zaadul Ma’ad (1/453) chapa ya Ar-Risaalah]

 

Ninasema: “Utendaji sahihi zaidi wa Swalaah hii ni kufanya rukuu mbili katika kila rakaa kama walivyosema Jamhuri kutokana na uwazi wa Hadiyth Swahiyh husika. Ama dalili za Abu Haniyfah na waliokubaliana naye, dalili hizi zimetaja rakaa mbili bila uainisho wakati Hadiyth za kundi la kwanza zimeainisha”.

 

Ama Hadiyth ya An-Nu’umaan bin Bashiyr kuhusu Swalaah ya rakaa mbili mbili, Al-Haafidh anasema katika mjalada wa tatu wa kitabu cha Al-Fat-h kwamba ikiwa Hadiyth hii imehifadhiwa, maana ya neno lake “rakaa mbili mbili” inaweza kuchukuliwa kama rukuu mbili. Ninasema: “Tushajua kwamba Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, hivyo hatuhitajii taawili yoyote”.

 

Ama riwaya zinazozungumzia kuhusu ziada ya rukuu mbili katika rakaa moja, Sheikh wa Uislamu (18/17-18) amesema kwamba hili limepewa udhaifu na Maulamaa weledi wanaosema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuswali Kusuwf isipokuwa mara moja tu siku alipofariki mwanaye Ibraahiym, na mwanaye huyu hakufa mara mbili, na wala hakuwa na Ibraahiym wawili. Isitoshe, imepokelewa kwa njia ya Tawaatur kwamba Nabiy aliswali Kusuwf siku hiyo kwa rukuu mbili katika kila rakaa.

 

Al-‘Allaamah Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (3/132) amesema: “Kauli ya mwisho kuhusiana na Swalaah ya Kusuwf ni kwamba lililo sahihi thabiti toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kuwa Swalaah hii ni rakaa mbili, na kila rakaa ina rukuu mbili. Na haya yamethibiti toka kwa Maswahaba wengi yakielezewa kwenye vitabu vinavyoaminika, njia na riwaya mbalimbali.  Ama kinyume na hayo, basi yatakuwa ima Dhwa’iyf au Shaadh, na hayafai kwa hoja”.


 Inaendelea...


Na Allaah anajua zaidi 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Eda: Maana ya Eda, Hikma ya Eda , Hukmu zake, Mambo yanayopasa na uyasiyopasa kwa mwenye Eda

Namna ya Kuswali Swalat Kusuwf (Swalah ya Kupatwa kwa Jua/Mwezi

Ramadhwaan ni Mwezi wa Du’aa na Du’aa hutakabaliwa