SWALAAT AL-ISTIKHAARAH
SWALAAT AL-ISTIKHAARAH
Imaam Masjid Tawbah: Kitaab Fiqh'i Sunnah-Mlango wa Swalah
SWALAAT AL-ISTIKHAARAH
Maana ya Istikhaarah
✅Istikhaarah maana yake ni kuomba uchaguzi au aumuzi katika jambo.
➡️Na Swalaah ya Istikhaarah hakika ni zawadi kubwa tuliyopewa sisi Umma wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani ina faida kubwa sana kwetu kwani hatuamui jambo letu tunaloliomba katika Swalaah hii, ila baada ya kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuongoze Yeye hilo jambo kama lina kheri na sisi Atufanikishe nalo na kama ni la shari Atuepushe nalo.
✅Yeye Pekee Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Mwenye kujua ya ghayb yaani yatakayotokea siku za mbele.
Idadi za Rakaa na Wakati wa Kuiswali Swalaat Al-Istakhaarah
✅Swalaah ya Istikhaarah ni raka'ah mbili na haina Suwrah maalumu na huswaliwa siku yoyote, wakati wowote na mara zozote unapopenda kufanya jambo hadi hilo jambo ujaaliwe kulifanya au usijaaliwe itakuwa yote ni kheri kwani madamu tu umeshaswali Istikhaarah basi umeshamuelekea Rabb wako kutaka Yeye Akuongoze. Kwa hiyo hata ukiswali mara moja tu inatosha kabisa kuwa umeshatimiza Istikhaarah.
✅Kwahiyo Mwenye kutaka kufanya jambo la halali, kisha akawa na shakashaka kama litakuwa na kheri ndani yake au litakuwa sawa, basi imesuniwa kwake aswali rakaa mbili zisizo za faradhi - rakaa zozote mbili hata kama ni katika Sunnah za rawaatib – kisha aombe baada ya kuziswali kwa du’aa iliyokuja katika Hadiyth ifuatayo:
Imepokelewa toka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatufundisha istikhaarah katika mambo yote. Aidha, anatufundisha Suwrah ya Qur-aan anasema:
((Akiazimia mmoja wenu kufanya jambo, basi aswali rakaa mbili zisizo za faradhi, kisha aseme: Allaahumma inniy astakhiyruka bi’ilmika, wa astaqdiruka biqudratika, wa as-aluka min fadwlikal Adhwiym, fainnaka Taqdiru walaa aqdiru, wa Ta’alamu walaa a’alamu, wa Anta ‘Allaamul Ghuyuub. Allaahumma in Kunta Ta’alamu anna haadhaal amra (atalitaja) khayrun liy fiy diyniy wa ma’aashiy wa ‘aaqibati amriy (au atasema: ‘aajilihi wa aajilihi) Faqdirhu liy wa Yassirhu liy, thumma Baariyki liy fiyhi. Wain Kunta Ta’alamu anna haadhal amra sharrun liy fiy diyniy wa ma’aashiy wa ‘aaqibati amriy (au atasema: ‘aajilihi wa aajilihi) Faswrifhu ‘anniy Waswrifniy ‘anhu, Waqdir liy al khayra haythu kaana, thumma Irdhwiniy bihi”.
↪️Rejea Hadiythi Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (719).
TANBIH/ANGALIZO KUHUSU SWALAAT AL-ISTIKHAARAH
✅Naam Zifuatazo ni tanbihi ambazo inabidi zizingatiwe⤵️
1️⃣Istikhaarah hufanywa wakati mtu anapoazimia kufanya jambo la halali, na haifanywi katika mambo ya halali ila kwa ajili ya kuchagua la kheri zaidi kati yake. Pia haifanywi katika mambo ya wajibu au ya haramu.
2️⃣“Baada ya kuiswali, inatakikana mtu alifanye lile ambalo anakuta kifua chake kimefunguka kwalo, asiutegemee ukunjufu aliokuwa ameulemea kabla ya kuswali, bali aliache chaguo lake moja kwa moja. Na kama si hivyo, basi atakuwa hamfanyii istikhaarah Allaah bali hawaa ya nafsi yake, na anaweza asiwe mkweli katika kuiomba kwake kheri na kujivua na ujuzi na uwezo na kuuthibitisha kwa Allaah Mtukufu. Akiwa mkweli katika hilo, atajivua uwezo, nguvu na chaguo lake mwenyewe.”
↪️Yamenukuliwa haya kutoka Naylul Awtwaar (3/90) toka kwa An Nawawiy.
3️⃣Si lazima aliyefanya istikhaarah aone njozi usingizini kama wanavyoitakidi watu wengi, bali inakuwa ni kwa lile ambalo kifua chake mtu kitalikunjukia, au jambo hilo litarahisishwa kwake kwa mujibu wa Alivyolikadiria Allaah.
4️⃣Chaguo la Allaah(Subhaanahu wa Ta'ala ) linaweza kuja kinyume na mtu anavyotaka au kwa lile ambalo analiona kama ni shari. Hapa ni lazima asalimishe jambo lake kwa Allaah.
(( كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ))
((Mmeandikiwa shariy’ah kupigana vita nako kunachukiza mno kwenu. Na asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni khayr kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui)).
↪️Suraat Al-Baqarah Aya ya 216.
5️⃣Istikhaarah ni du’aa, hakuna ubaya kuikariri.
Tanbihi/Tahadhari
Kuna Hadiythi isemayo:
(( إذا هممت بأمر فاستخر ربك فيه سبع مرات))
((Ukiazimia jambo, basi mfanyie istikhaarah Mola wako mara saba)).
Hadiythi hii ni batili na haifai.
DUA YA SWALAAT AL-ISTIKHAARAH
➡️Naam katika Hadiythi Mtume Muhammad ( Swalla Allaahu ‘ alayhi wa sallam ) amesema ⤵️
عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنهما، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُعَلِّمُنَا الِاسْتِخَارَةَ فِي الأُمُورِ كُلِّهَا، كَمَا يُعَلِّمُنَا السُّورَةَ مِنَ القُرْآنِ يَقُولُ: إِذَا هَمَّ أَحَدُكُمْ بِالأَمْرِ فَلْيَرْكَعْ رَكْعَتَيْنِ مِنْ غَيْرِ الفَرِيضَةِ، ثُمَّ لِيَقُلْ:
”Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anha) amesimulia kwa kusema:
”Mtume wa Allaah alikuwa akitufundisha Istikhaarah katika mambo yote kama vile anavyotufunza Suurah ndani ya Qur-aan. Akisema: ”Mmoja wenu akikusudia kufanya jambo, basi aswali Rak´ah mbili zisizo za faradhi, kisha aseme⤵️
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْتَخِيرُكَ بِعِلْمِكَ، وَأَسْتَقْدِرُكَ بِقُدْرَتِكَ، وَأَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ العَظِيمِ، فَإِنَّكَ تَقْدِرُ وَلاَ أَقْدِرُ، وَتَعْلَمُ وَلاَ أَعْلَمُ، وَأَنْتَ عَلَّامُ الغُيُوبِ، اللَّهُمَّ إِنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الأَمْرَ خَيْرٌ لِي فِي دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي – أَوْ قَالَ: عَاجِلِ أَمْرِي وَآجِلِهِ – فَاقْدُرْهُ لِي، وَيَسِّرْهُ لِي، ثُمَّ بَارِكْ لِي فِيهِ، وَإِنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الأَمْرَ شَرٌّ لِي فِي دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي – أَوْ قَالَ عَاجِلِ وَآجِلِهِ – فَاصْرِفْهُ عَنِّي، وَاصْرِفْنِي عَنْهُ، وَاقْدُرْ لِي الخَيْرَ حَيْثُ كَانَ، ثُمَّ أَرْضِنِي به
”Ee Allaah! Hakika mimi nakutaka ushauri kwa ujuzi Wako na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako na nakuomba kutokana na fadhilah Zako tukufu. Hakika Wewe unaweza, nami siwezi, unajua, nami sijui Nawe ni mjuzi wa yaliyofichikana. Ee Allaah! Iwapo unajua kuwa jambo hili lina kheri nami katika dini yangu, maisha yangu na mwisho wa jambo langu” – au alisema: ”Duniani na Aakhirah” – basi nakuomba uniwezeshe nilipate na unifanyie wepesi kisha unibarikie kwacho. Endapo unajua kwamba jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu, maisha yangu na mwisho wa jambo langu, basi liweke mbali nami, uniepushe nalo na nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, halafu niridhishe kwalo.”
↪️Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy (07/162) nambari (1162).
✅Hajuti yule mwenye kumtaka Allaah ushauri, akawashauri waja waumini na akawa imara katika jambo lake.
➡️Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema⤵️
وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ
”Washauri katika mambo na unapoazimia, basi mtegemee Allaah. Hakika Allaah anawapenda wanaotegemea.”
↪️Suraat Al-Imraan Aya ya 159.
Rejea pia Kitaab Rejea Kitaab Huswn-ul-Muslim.
Tutaendelea Wiki Ijayo In Shaa Allaah....
Unaruhusiwa Kusambaza, Kuwa Muadilifu, Tafadhali Usibadili Chochote
Imeandaliwa na Imaam Masjid Tawbah
Maoni
Chapisha Maoni