Panaotakiwa kutolewa Zakaah

 PANAPOWAJIBIKA KUTOA ZAKAAH

Naam inawajibika kuitoa Zakaah wakati wake unapowadia, na haijuzu kuichelewesha isipokuwa kwa dharura inayokubalika.

 

Kutoka kwa Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema kuwa; Nabiy (Swalla Alaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"Haichanganyiki mali pamoja na Zakaah isipokuwa itaiangamiza", na katika riwaya nyingine;

 

"Inakuwa ishakuwajibikia katika mali yako kuitolea Zakaah, kisha usiitoe, kwa hivyo (mali ya) haramu (isiyotolewa Zakaah) inaiangamiza (mali ya) halali". [Ash-Shaafi’iy na Al-Bukhaariy katika 'At-Taariykh']


Na Allaah anajua zaidi 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Eda: Maana ya Eda, Hikma ya Eda , Hukmu zake, Mambo yanayopasa na uyasiyopasa kwa mwenye Eda

Namna ya Kuswali Swalat Kusuwf (Swalah ya Kupatwa kwa Jua/Mwezi

Ramadhwaan ni Mwezi wa Du’aa na Du’aa hutakabaliwa