Niyah wakati wa Kutoa Zakaah
NIYAH WAKATI WA KUTOA ZAKAAH
Zakaah ni ‘Ibaadah, na kwa ajili hiyo kutia Niyyah ni jambo muhimu kama ilivyo katika ‘Ibaadah yoyote ile.
Na Niyah ni kitu cha moyoni na hakina uhusiano na ulimi, na kusudi lake ni kuwa mtu anapotoa Zakaah akusudie kuitoa kwa ajili ya Allaah.
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"Hakika ya amali yoyote ni kutokana na Niyyah, na mtu hulipwa kutokana na Niyyah yake".
Na Allaah anajua zaidi
Maoni
Chapisha Maoni